Tuesday 20 August 2013

KANISA KATOLIKI PAROKIA YA MAFINGA


“Bikira Maria Aliyepalizwa Mbinguni”


“JIMBO LA IRINGA”
UTANGULIZI
1.   Parokia ya Mafinga ni Parokia ya Jimbo la Iringa  upande wa Kaskasini-Kusini ya Tanzania, kwenye barabara kuu kutoka Dar Es Salaam kuenda Zambia.
2.    Parokia ya Mafinga ina umbali wa kilomita 80 kutoka Jimboni
3.    Parokia ya Mafinga inapakana na parokia zifuatazo;
       Kaskasini; Parokia ya Sadani
       Kusini; Parokia ya Mdabulo, Parokia ya Kibao
       Mashariki; Parokia ya Lyasa, Parokia ya Ulete
       Magharibi; , Parokia ya Nyololo,
4.    Parokia ya Mafinga ina wakazi 55.866
5.    Parokia ya Mafinga ina Wakatoliki 9.548
6.    Katika eneo la Parokia ya Mafinga kuna madhehebu yafuatayo;
       Waluteri, Waanglikana, Wamoravian, Kanisa la Pentekoste
7.    Parokia ya Mafinga ina vigango 17, navyo ni;
CHANGARAWE11 km
 NDOLEZI 09 km
ISALAVANU22 km
MAMBA18 km
MTULA16 km
ULOLE35 km
MATANANA32 km
IHEFU18 km
IRUNDI33 km
ITALAVANU11 km
IKONGOSI18 km
MTIRI19 km
IFWAGI27 km
IKONONGO29 km
SAO HILL12 km
ISUPIRO10 km
SAO HILL12 km
 8.  Katika Parokia nzima ya Mafinga kuna Misa 10 kila Jumapili.
- Parokiani Misa 3 (saa 1.00-Misa ya kwanza,saa 3.00-Misa ya pili, 5.15-Misa ya tatu). Wanaoshiriki Misa Parokiani kila Jumapili ni waamini takriban 3.000.
- Vigangoni Misa 7(Kama kawaida kila padre anasali Misa 2 vigangoni; Misa katika kigango cha kwanza saa 3.00, Misa katika kigango cha pili ni saa 5.00. Wanaoshiriki Misa katika vigango saba  ni takriban 1000.
- Waamini wa vigangoni wanapata Misa mara mbili kwa mwezi.
JINA LA PAROKIA
1.   Parokia ya Mafinga huko nyuma mnamo mwaka 1953 iliitwa PAROKIA YA MAKALALA kadiri ya jina la eneo lile. Mapadre Wakonsolata waliamua kuipa Parokia jina la msimamizi wake ‘BIKIRA MARIA ALIYEPALIZWA MBINGUNI’.
2.    Makabila yanayopatikana katika Parokia ya Mafinga ni kwa asilimia kubwa  WAHEHE; makabila mengine ni; Wabena, Wakinga, Wangoni, Wanyakyusa na wengineo.
3.    Kabila lenye watu wengi zaidi ni WAHEHE.

0 comments: