Friday 30 August 2013

WAKO WAPI MABWANA NA MABIBI AFYA?

Nikiwa eneo moja ndani ya jiji la Mbeya nikipata chakula cha mchana katika kibanda kimoja cha chipsi na marafiki zangu. Mmoja wetu akaanzisha zogo ambalo haliku malizika mpaka nikaona niandike hii makala fupi. Jamaa aliuliza Wapo wapi mabwana na mabibi Afya?. Yawezekana jamaa alipata wazo hilo kutoka na mahali tulipokuwepo  (Kibanda cha chipsi) . Zamani mimi mwenyewe niliwashuhudia viongozi hawa muhimu wakifuatilia nyumba kwa nyumba kama kuna huduma muhimu kama choo, shimo la taka, mifereji ya maji taka nk. Lakini kwa kipindi fulani mpaka siku za hizi karibuni hawa wahudumu mbona hawaonekani wala kusikika? Wapo wapi? Vipi mbona hakuna mtu anayefuatilia usafi wa maeneo ya migahawa na vibanda vya chipsi? Mama kajifungua miezi michache na anaendelea na kazi ya MAMA LISHE au Kijana akiwa na nguo inayoacha  kwapa zake nje  anatoa huduma ya chakula. Vijijini wengi hawana vyoo au mashimo na mifereji ya maji taka. Mijini nako madampo yapo lakin taka hazipelekwi kunakohusika. WAKO WAPI MABWANA NA MABIBI AFYA? Je, wapo? au wapo wa Kichina (feki)? Au kitengo hiki cha Mabwana na Mabibi Afya Hakipo tena?

JE TUNAHITAJI ZIARA YA OBAMA ILI KUONDOA TAKA KAMA HIZI?

0 comments: