Ajali mbaya imetokea eneo la Tungi (5Km kutoka Morogoro) barabara ielekeayo Dar es Salam. Ajali hiyo imetokea leo muda wa saa 11 jioni iliyohusisha basi la Majinja lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam na Lori lililokuwa likitokea Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wakiwemo abiria walionusurika dereva wa basi la Majinja alikuwa aki overtake Lori jingine na mbele yake kukawa na Lori jingine, hivyo ilipelekea basi la Majinja kuligonga Lori kwa mbele kabla ya kuanguka pembeni mwa barabara. Hakuna yeyote aliyeripotiwa kupoteza maisha licha ya kuwepo kwa abiria wengi waliopata maheraha ambao walipata msaada wa kukimbzwa hospitali Morogoro.
Monday, 13 May 2013
AJALI ... TUNGI MOROGORO
Monday, May 13, 2013
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment